Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) akikabidhiwa fomu ya kugombe nafasi ya Urais na Katibu wa Chama hicho wa Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, Kassim Chogamawano, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo mchana kwenye Ofisi ya Chama hicho Tawi wa Mnazi Mageuzi iliyopo Temeke jijini. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Wilaya ya Kinondoni, Juma Nkumbi.
Profesa. Lipumba akifurahia fomu yake baada ya kukabidhiwa.
Prof. Lipumba akisalimiana na Mzee wa Chama hicho kwa bashasha na furaha za hali ya juu wakati alipofika kuchukua fomu hiyo.
Mwenyekiti na Katibu, wakikagua Kadi ya Uanachama ya Prof. Lipumba kabla ya kumkabidhi Fomu.
Baada ya kukaguliwa furaha ya mzee huyo ilirejea tena kwani aliruka na kumkumbatia huku wakifurahi kwa pamoja na kufanya umati wa wanachama lukuki waliokuwapo mahala hapo kuangua kicheko cha furaha na vigelegele.
Hawa ni sehemu tu ya Wanachama wa CUF, waliokusanyika nje ya ofisi ya Chama hicho Temeke, kumshuhudia mwenyekiti wao akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Hapa ni wakati Lipumba akipokelewa kuingia kwenye Ofisi za Chama hicho.
Hapa ni wakati Mwenyekiti wa Chama hicho Tawi la Mnazi Mageuzi, Azizi Ngamwembe (kushoto) akimkabidhi kitita cha fedha Sh. 500,000, zilizochangwa na wanachama, kwa ajili ya kumsaidia kulipia Fomu ya kuwania nafasi ya urais.
Prof. Lipumba, akiwasalimia Wanachama wake waliokuwapo eneo hilo wakisubiri kushuhudia zoezi hilo la kukabidhiwa fedha na fomu.
No comments:
Post a Comment