Habari za Punde

*MAPOKEZI YA DK. BILAL BAGAMOYO LEO

Msafara wa Waendesha Pikipiki wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa wakimpokea Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwasili Bagamoyo kwa ajili ya kufanya mkutano wa Kampeni leo jioni na kwanadi wagombea ubunge Shukuru Kawambwa wa Jimbo la Bagamoyo na Amour Abuu Jumaa wa Jimbo la Kibaha Vijijini.
Umati wa wakazi wa Bagamoyo, wakijipanga kusubiri kumpokea Mgombea Mwenza Dk. Bilal wakati alipokuwa akiingia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo leo jioni.
Wasanii wa Kikundi cha Sprendid, wakionyesha umahiri wao wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza Dk. Bilal alipofika katika uwanja huo kufanya mkutano wa kampeni.
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Sauda Mpambaliyoto na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bagamoyo, Shukuru Kawambwa, wakisakata ngoma na msanii wa kikundi cha Sprendid wakati wa hafla ya mkutano huo leo.
Rubani wa ndege ya kukodi anayeendesha ndege inayomsafirisha mgombea Mwenza Dk. Bilal, David Ellis (kushoto) akizungumza na Dk baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Slaam akitokea Kisiwa cha Mafia, kwa ajili ya kuanza safari ya Bagamoyo.
Dk. Bilal akiagana na Rubani huyo, David Ellis baada ya kuwasili leo.....






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.