Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa Shirikisho hilo, Leodger Tenga, aliwataja watu walioteuliwa na kamati hiyo, ambao mbali na Osiah kuwa Katibu Mkuu pia, alimtaja Boniface Wambura, kuteuliwa kushika nafasi ya Frolian Kaijage, yaani Ofisa Habari wa Shirikisho hilo.
Aidha alisema kuwa uteuzi huo umekuja baada ya nafasi hizo kuachwa wazi kwa muda mrefu, baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Frederick Mwakalebela, kuiacha nafasi hiyo baada ya kumaliza muda wake na kuingia rasmi katika Siasa na kuwania Ubunge wa Jimbo la Iringa mjini, kupitia tiketi ya CCM.
Kuhusu nafasi ya Ofisa Habari imekuja baada ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo, Florean Kaijage, pia kumaliza muda wake.
Alisema kuwa jumla ya maombi 64, ya nafasi ya Katibu Mkuu yalipokewa na shirikisho hilo, ambapo nafasi ya Ofisa Habari waombaji walikuwa 44 na 17 kati ya hao walipiota katika mchujo wa mwanzo wa nafasi ya Katibu Mkuu.
Pia 11 walifanikiwa kupita katika nafasi ya Ofisa Habari, na walioitikia wito wa kufanyiwa usahiri, walikuwa ni 15 kwa nafasi ya Katibu Mkuu na 10 kwa nafasi ya Ofisa Habari, ambapo hadi mwisho majina matano bora kwa kila nafasi yalipokewa na Kamati ya Utendaji.
Aliwataja watu wengine walioteuliwa na Kamati hiyo kuwa ni James Kabwe, aliyeteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Masoko wa TFF.
No comments:
Post a Comment