Wachezaji wa Kilimanjaro Stars, wakishangilia ushindi na mchezaji wa timu hiyo, Mrisho Ngasa (kulia) aliyekuwa na kadi mbili za njano na kumsababishi kutocheza mchezo huo wa fainali, hapa akiwapongeza wenzake na kucheza nao Kiduku.
Askari Polisi, wakimtoa shabiki aliyevamia uwanjani wakati mchezo huo ukiendelea, kwa furaha.
Wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, wakishangilia na Kombe lao baada ya kukabidhiwa kombe hilo kwa kuwafunga Ivory Coast katika mchezo wa CECAFA Tusker Challenge Cup, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Goli la kuongoza na la ushindi la Kilimanjaro Stars, lilifungwa kipindi cha kwanza na beki wa kulia wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa kwa njia ya penati goli lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo. Mbali na kombe hilo pia timu hiyo imekabidhiwa hundi ya Sh 30, 000 za kimarekani.
No comments:
Post a Comment