Habari za Punde

*KILIMANJARO STARS YATINGA FAINALI KOMBE LA TUSKER CHALLENGE

Beki wa Shadrack Nsajigwa (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Uganda, wakati wa mchezo wa kombe la Tusker uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Kilimanjaro Stars imeibuka na ushindi wa mabao 5-4.
Timu hizo zimeweza kumenyana na kumaliza dakika 90 bila kufungana, na hatimaye kuongezwa dakika 30, ambazo nazo zimeweza kumalizika bila timu hizo kufungana na kufanya timu hizo kuingia kwenye hatua ya kupigiana mikwaju.
Katika hatua hiyo Juma Kaseja ameweza kuwainua mashabiki lukuki waliokusanyika uwanjani hapo na kuwahiza kushangilia na kisha kupangua mkwaju mmoja wa penati huku wachezaji wa Kilimanjaro wote wakipiga na kufunga penati.
Kwa hatua hiyo sasa Kilimanjaro Stars itakipiga na Ivory Coast katika fainali hizo, mchezo utakaochezwa jumapili katika uwanja huo huo wa Taifa, ambapo Ivory Coast wamepenya na kuingia fainali baada ya kuwafunga Ethiopia mchezo iliochezwa leo kabla ya mchezo wa Kilimanjaro na Uganda. Wapigaji wa penati kwa upande wa Kilimanjaro walikuwa ni, Shadrack Nsajigwa, aliyepiga penati ya kwanza, Stephano Mwasika, Shaaban Nditi, Salum Machaku na yamwisho ikakandamizwa na Erasto Nyoni na kuwainua mashabiki.
Kipa wa Uganda, akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake wakati wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.