Habari za Punde

*TASWA FC KUSHIRIKI SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR

Hashim Salum, mratibu wa mashindano ya Kombe la mapinduzi Zanzibar.
TIMU ya waandishi wa habari za michezo nchini TASWA Fc, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar siku ya fainali za Kombe la Mapinduzi zitakazofanyika uwanja wa Amani mjini Zanzibar Januari 12 mwakani.

Michuano hiyo inayotarajia kushirikisha jumla ya timu nane itafikia kilele na kufikia hatua ya fainali Januari 12, ambapo katika mchezo huo wa fainali timu ya TASWA Fc, inatarajia kucheza na wawakilishi hao ikiwa ni mchezo wa utangulizi kabla ya kuanza kwa mtanange huo wa fainali.

“Mchezo wa kwanza unatarajia kuwa kati ya timu ya Veterani wa Tanzania Bara na Veterani wa Zanzibar utakaochezwa January 11 kwenye Uwanja wa Mau tse Tung”, alisema Kazi

Akizungumza na Sufianimafoto, mratibu wa michuano hiyo kupitia Kampuni ya Popular Sports & Entertinment, Othman Kazi, alisema kuwa maandalizi yanaendelea na kwamba bado wanaendelea kufanya mazungumzo na timu za Yanga, Simba, Mtibwa na Azam ili ziweze kukubali kushiriki michuano hiyo.

Aidha alisema kuwa timu ambazo tayari zimekwisha thibitisha kushiriki michuano hiyo kutoa Visiwa vya Zanzibar ni pamoja na Zanzibar Ocean View, Jamhuri na Kmkm.

Naye Mratibu wa michuano hiyo kwa upande wa Zanzibar. Hashim Salum, alisema kuwa maandalizi ya sherehe hizo za mapinduzi Zanzibar, yamekamilika na kuongeza kuwa mbali na burudani ya mchezo wa soka pia inatarajiwa kua na burudani mbalimbali za kupamba sherehe hizo.

Akizungumza na Sufianimafoto, Mwenyekiti wa TASWA Fc, Majuto Omar, alisema kuwa timu ya yake imepokea mwaliko huo na tayari imeshaanza mazoezi ya pamoja ya jioni katikati ya wiki kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo, mbali na mazoezi ya kila jumamosi.

Timu hiyo inatarajia kuondoka Dar es Salaam Januari 11, ikiwa na msafara wa watu 20 kuelekea Visiwani Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.