Habari za Punde

*TBL YAKABIDHI ZAWADI ZA WASHIRIKI WA BONGO STAR SEARCH

Mshindi wa BSS kujinyakulia kitita cha Sh milioni 30.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production, Ritha Poulsen, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, wakati wa utambulisho wa wasanii walioingia hatua ya tano bora watakaopanda jukwaani Desemba 17 kuwania taji la Bongo Star Search. Katikati ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe na Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA, Vicky Temu.

Wasanii watano Bora wanaotarajia kupanda jukwaani Desemba 17, kuwania taji la Bongo Star Search, kutoka (kushoto) james Martine, Joseph Payne, Mariam Mohammed, Waziri Salum na Bella Kombo, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi walipokuwa wakitambulishwa kwenye mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam leo mchana.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kulia) akimkabidhi hundi ya Sh. Milioni 30, Mkurugenzi wa Benchmark Production, Ritha Paulsen, kwa ajili ya zawadi ya mshindi wa kwanza wa shindano hilo, linalotarajia kufanyika Desemba 17 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Mwenge Dar es Salaam.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.