Habari za Punde

*KIKOMBE KILIANZIA KWA BABU LOLIONDO, AKAJA DOGO WA MBEYA NA SASA TABORA

Umati wa wagonjwa Ukisubiri kikombe cha Dada, Mkoai Tabora.

Baada ya Babu Loliondo, Mangi Tarakea na Dogo wa Mbeya, mtu mwingine ameibuka safari hii huko mkoani Tabora, akitoa kikombe anachodai kinatibu maradhi sugu, na kuvutia umati mkubwa wa watu wa mji huo mkongwe.



Dada Magreth Mutalemwa, mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora mjini, amejitokeza na kudai alioteshwa kutibu watu na Bikira Maria, mpaka sasa OCD yupo hapo kwa dada na amemwambia mdau wa libeneke la kerongingi, Mkala Fundikira, kuwa yeye alishapata kikombe toka kwa dada na amejitapa hatoondoka mahala hapo mpaka askari zaidi watakapowasili kuongeza ulinzi.



Watu kadhaa wameonesha imani na dawa ya dada na kusema wana nafuu tangu wanywe dawa yake ambayo bado haijafahamika chanzo ama mchanganyiko wake.


Kamati ya ulinzi na usalama itakaa muda mfupi kujipanga na mfumuko wa watu watakaokuja kufuta huduma ya dada Magreth Mutalemwa.


Kwa mwendelezo huu sasa haifahamiki kuwa ni dawa za kweli na je ni kweli wanaoteshwa kama ambavyo alioteshwa Babu ana ni uchu wa kujipatia fedha tu.


Haya yote yanawezekana ila wananchi wametokea kuamini zaidi imani kiasi kwamba hata Sufianimafoto naye akiamua kutangaza kuwa ameoteshwa usiku kutoa dawa hiyo, basi wananchi wataamini na kusitisha safari za Loliondo na kuanza foleni mpya ya Dar, jamani wananchi tuwe makini tunakoelekea sasa tunaweza kunyweshwa hata kisichostahili kuywewa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.