Vijana wanauza nguo za mitumba wakikatiza katika mitaa ya mjini Songea mkoani ruvuma leo wakitafuta wateja wa nguo hizo. Vijana wengi wameanza kutembeza biashara hiyo ya nguo katika mitaa ya songea baada ya kubomolewa Vibanda vyao vya biashara na Manispaa ya Songea kutokana na vibanda hivyo kujengwa bila kufuata utaratibu ili kuweka manispaa hiyo katika hali ya usafi. Picha Zote na Muhidin Amri, Songea
Wachuuzi wa nguo kuukuu (mitumba) ambao hawakufahamika majina yao wakitafuta wateja katika mtaa wa mpate mjini Songea kama walivyonaswa na kamera yetu.
Mfanyabiashara wa viatu vya mitumba katika mtaa wa Sokoni mjini Songea Bakari Ali,akipanga viatu hivyo kwa ajili ya kuwavutia wateja wanaopita katika mtaa huo.
No comments:
Post a Comment