Na Boniface Wambura, Lagos
Awali U23 ilikuwa ifike nchini humo saa 4 kamili asubuhi, lakini ikachelewa kutoka Nairobi ambapo ilitoka saa 3.30 badala ya saa 1.30 baada ya ndege ya Kenya Airways kuchelewa kuondoka.
Kocha Jamhuri Kihwelo amesema vijana wake katika hali nzuri ya kupeperusha
bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambapo mshindi baada ya matokeo ya
nyumbani ambapo U23 ilipata ushindi wa bao moja ataingia katika hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kuiwakilisha Afrika katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini London, Uingereza.
Amesema timu yake itacheza mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza huku akijaza viungo wengi kwa lengo la kumiliki mpira kwa muda mrefu, hivyo kuzuia
mashambulizi ya timu pinzani kwa staili.
Kihwelo amesema mbele atatumia washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata.
Wachezaji wengine aliokuja nao hapa ni Jamal Mnyate, Jackson Wandwi, Hussein
Javu, Mohamed Soud, Obadia Mungusa, Abuu Ubwa, Juma Abdul, Abdul Juma, Himid Mao, Issa Rashid, Khamis Mcha, Salum Abubakar, Shomari Kapombe, Jabir Aziz, Godfrey Wambura na Awadh Juma.
No comments:
Post a Comment