Habari za Punde

*JICHO LA SUFIANIMAFOTO NEW YORK CITY

Hili ni eneo maarufu sana New York 'Time Square' ni eneo maarufu na lenye historia katika Visiwa vya New York, ambapo kila mwisho wa mwaka hufanyika sherehe kubwa 'Ball Drop' inayofanya mjumuiko wa watu wengi kutoka jiji la New York na Vitongoji vyake pamoja na State nyingine, na baada ya kuangushwa mpira huo watu wote walioeneo hilo kwa siku na muda huo hushangilia ikiwa ni ishara ya kuuanza mwaka mpya. Wanasema eti kama umefika New York na hukubahatika kufika mahala hapa basi umekosa kujua mengi kuhusu mji huu na unakuwa hujafika Marekani
Ni Baadhi ya majengo marefu yaliyo katika eneo hilo la Time Square.
Moja kati ya madaraja matatu maarufu yaliyokatiza juu ya mto ulio katikati ya mji huo, ni Daraja maarufu la Manhattan, ambapo mfano wa daraja kama hili eti ndiyo linatarajia kujengwa kigamboni.....
Ni Baadhi ya Majengo marefu yaliyo katikati ya mji huo, wenyewe husema 'Vibirirti'
Sufianimafoto akipozi kwa picha nje ya Jengo la UN.
Huyu jamaa ni mshikaji wangu tu ambaye tulikutana katika duka moja huku kila mmoja akiwa na kamera mkononi jambo ambalo lilituvutia wote na kuamua kupigana picha za mapozi eti yeye hili ndiyo pozi lake, ebwana eeh! alimchekesha kila mmoja aliyekuwapo dukani hapo.
Hii ni folrni ya Abiria wanaosubiri kupanda Tax, ambapo Tax hizo zenye rangi ya njano hupakia kwa foleni na abiria hufuata foleni kwa heshima zote hadi inapofikia zamu yake.
Hata Ulaya wapo ombaomba kama Bongo, ila tofauti waha huwa ni wasafi na kutembea na mabegi yao ya nguo kama wanavyoonekana pichani wanaonekana ni mtu na mkewe, wakiuchapa usingizi mchana kweupe tena katika jua kali baada ya kuzurula na kazi hiyo, hapa ni mapumziko baadaye kazi inaendelea......
New York, Madada wengi wamekuwa wakifuga mbwa na wamekuwa wakizunguka nao mtaani na 'kuwaendo' kama watoto, hii imeelezwa kuwa hawa ni baadhi ya madada ambao huishi 'Alone' hivyo hufuga mbwa ili kuwakeep bize na kuwaondoa upweke ndani ya nyumba, ambapo ukipita katika mitaa ya jiji la New York unaweza kujikuta ukicheka kimoyomoyo kwa jinsi utakavyokutana na aina za vijimbwa vingine ni vidogo kama Panya na vingine vinasura za ajabu hasa na vingine vimenyolewa manyoya yote na kuachwa nysi tu kiasi ukipishana naye huachi kugeuka na kumuangalia.
Yeye huyu ameamua kujifugia Jimbwa kubwa kama Mbuzi.

Lakini Mbwa hawa imeelezwa kuwa wanagharama zaidi hata ya binadamu kwa jinsi wanavyotakiwa kuwahudumia, ambapo wengine hulala nao kitandani, na kuwatoa kukojoa kila bada ya muda fulani kulinganana jinsi alivyomzoesha mbwa wake, na kila mbwa mmoja hugharimu zaidi ya Dola 1000 kwa mwezi na pia ni lazima kila jioni ama asubuhi umtoe mbwa wako na kumtembeza katika mitaa na kumrudisha
Haya ni matangazo ya biashara...
Mdada huyu (kushoto) si chizi wala si omba omba bali ni mmoja kati ya wanaofanya kazi ya kutangaza biashara za katika maduka na kugawa vipeperushi kwa wapita njia, ambapo hulipwa kwa masaa. Na ili kuwavutia watu ili wakushangae na waweze kuwa makini kukusikiliza ni kama hivi kujigeuza uhalisia wako.
Huyu ni Askari wa kike wa Usalama Barabarani, akiongoza magari katika moja ya Barabara za Jiji la New York, huku akiwa amevalia 'Pensi' Je Dada zetu wa Bongo wataweza hii na je Mabosi zao wapo tayari kuwaruhusu na kuwaandalia Uniform za aina mbili Sketi na Kaptura ili waweze kuendana na mazingira ya kazi???? inapobidi kuvaa Sketi wavae na inapobidi kuvaa Pensi wavae.
Hizi ni sehemu za Barabara za jiji la New York zikiwa na Beria ambapo nyingine humilikuwa na Makampuni binafsi ambazo zimekuwa zikiwatoza madereva fedha kwa kila gari litakalovuka eneo hilo, Imeelezwa kuwa beria hizi zimejengwa maalum kwa ajili ya watu wanahitaji kukwepa foleni hulazimika kulipa ili kupita barabara hiyo isiyo na foleni. Kwa Staili hii kweli nchi itaacha kuwa na Maendeleo??? kwani kila kitu utakachonunua nchini humo ni lazima ukilipie kodi haijalishi ni fedha kiasi gani hadi Senri moja ya Dola ujue umelipia kodi bila we kujijua na hata mfanyabiashara ni ngumu kukwepa kulipa kodi anajikuta 'Automatic' amelipa kodi kupitia mwananchi.
Hii pia ni moja ya barabara nyingine ya aina hiyo.
Polisi wa Usalama Barabarani hukaa kila kona ya Barabara wakiwa na Gari, Pikipiki ama Bajaji kama hii, kiasi kwamba unapofanya kosa na ukakimbia huwezi fika mbali kabla ya kukamatwa kwani kila askari anawajibika katika kituo chake.
Na Dereva unapofanya kosa Leseni yako inapunguzwa alama fulani hadi zikimalizika kutoka Class uliyonayo unashitakiwa na kunyang'anywa leseni na kuzuiliwa kuendesha gari hadi utakapotimiza taratibu za kuomba upya leseni na kupata, kwa mtindo huu kila dereve ni lazima awe na adabu na kuhesimu sheria za usalama Barabarani.
Sufianimafoto akipozi kwa picha na Mshikaji wake Ibra. Ibra ni Mbongo anayeishi nchini Marekani katika Mitaa ya Manhattan, ambaye amekuwa na msaada mkubwa kwa wabongo wanaofika mji huo na kutaka muongozo ili kufanikisha mahitaji yao. Big Up Ibra, Wabongo mkihitaji kupata msaada wa kuwa na mwenyeji katika maeneo fulani mkifika jiji hili basi mnaweza kuwasiliana na Ibra kupitia nambza +1347 475 4313.
Ebwana eeh! Mtaa huu ni kama mtaa wa Kongo Bongo, kwani pilika pilika za watu katika mtaa huu hazikatiki.
Sufianimafoto (kushoto) akipozi na rafiki zake, Ibra (katikati) na Tahir Bilal, wanaoishi New York, baada ya kukutana nao kwa mara ya kwanza baada ya kuwasili nchini humo. Ibra anaishi Manhattan na Tahir anaishi Blooklyn.
Sufianimafoto, akipozi na mchizi wake ambaye ni askari wa Marekani katika jiji la New York, baada ya kukutana eneo la Time Square, akiwa katika lindo lake.
Eneo hili ndiyo hasa watu hukaa na kushangaa maajabu yaliyopo eneo la Time Square.
Hili ni sanamu la kumbukumbu la mtu maarufu New York, ambaye alikuwa akishona nguo za aina mbalimbali na za mitindo kwa kutumia Cherehani ya kusukuma kwa miguu, na mtaa huo umebaki na jina la Seven Fashion hadi hii leo.
Baada ya kubomolewa kwamajengo pacha katika tukio la Desemba 11, Sasa hili ndilo Jengo la 'Empire State Building' ambalo ni lefu kuliko yote Marekani lililobakia.
Sufianimafoto, akipita nje ya Jengo la ukumbi wa Madson Square, ambao ndiyo aliokuwa akipambania Mike Tyson na unaofanyika baadhi ya michezo mingine.
Kodi inaendelea kukusanywa........

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.