Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU 3 YA WANAWAKE WAJASILIAMALI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiliamali, yatakayowashirikisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fulsa kwa Wote (EOTF) na kudhaminiwa na Benki ya NBC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mshauri wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, Robi Matiko, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mgulani jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kufungua rasmi mafunzo ya siku tatu ya Wanawake wajasiliamali, yatakayowashirikisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fulsa kwa Wote (EOTF) na kudhaminiwa na Benki ya NBC. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo. Mwinda Kiula.
Wafanyakazi wa Benki ya NBC, Mshauri wa Mawasiliano katika benki hiyo, Robi Matiko (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula, wakiwa ndani ya ukumbi huo wakati wa ufunguzi wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.
Mmoja kati ya washiriki ambaye pia ni mjasiliamali wa katika Mafunzo hayo, Alya Riyami, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya ufunguzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zakhia Bilal, (wa pili kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mgulani jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiliamali yatakayowashirikisha wanawake wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fulsa kwa Wote (EOTF) na kudhaminiwa na Benki ya NBC. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko huo. Mama Anna Mkapa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.