Habari za Punde

*WAJUMBE WA MCT WAMREJESHA JAJI ROBERT KISANGA KUWAONGOZA TENA KWA MIAKA 3

WAJUMBE wa baraza la habari Tanzania (MCT) wamempitisha kwa kura za kishindo kwa mara nyingine Rais wa bodi ya MCT aliyemaliza muda wake, jaji Robart Kisanga, kuendelea kuongoza nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Wengine walioshinda kwa kishindo katika uchaguzi huo ni pamoja na makamu wa Rais wa MCT Chame Omari Omari kutoka Zanzibar kuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo na kupata kura zote 39 pamoja na Rais wa muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanznia (UTPC )Keneth Simbaya ambaye aliongoza kwa kura katika nafasi ya wajumbe wanne wa bodi ya MCT kupitia tasnia ya wanahabari nchini.

Simbaya ambaye ni mwenyekiti wa Iringa Prees Club alionyesha ni nyota ya katika mkutano huo kwa kushinda kwa kishindo nafasi hiyo kwa kupata kura (32) pamoja na awali jina lake kuenguliwa kabla ya kurejeshwa tena dakika za mwisho.

Katika uchaguzi huo kwa upande wa kundi la wagombea kutoka vyombo vya habari kura zilizopigwa ni 156 hakuna iliyoharibika na katika kundi hilo wagombea walikuwa ni 7 na watu wanne ndio walitakiwa Johnson Mbwambo(13) ,Rufii haji Makame(26), Rose Haji(27),Wallece Mauggo(20),Keneth Simbaya(32),Badra Masoud(22),Gadby Mgaya(16),

Mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huo Benny Mwaipaja aliwatangaza washindi ambao wamechaguliwa mbali ya Simbaya ni wengine ni ,Rufii haji Makame,Badra Masoud na Rose Haji.

Katika kundi la vyombo vya umma ambapo wagombea walikuwa na 6 kati ya watatu waliotakiwa wagombea hao na kura zao katika mabano ni pamoja na Prof Ruth Meena(31), wakili Alex Mgongolwa(16), Usu Mallya(21),Jaji Thomas Mihayo(23), Sultan Mundeme (8)na Alli Mufuruki (14).

Hata hivyo kinyang'anyiro kikali kilikuwa kati ya Jaji Thomas Mihayo na wakili maarufu wa kujitegemea Alex Mgongolwa ambao awali waligongana kwa kupata kura 19 wote hali iliyopelekea uchaguzi kurudiwa kwa wawili hao na kupelekea wakili Mgongolwa kushindwa kwa kupata kura 16 huku jaji Mihayo akipata kura 23 na Usu Mallya na Prof Ruth Meena.

Huku waliochaguliwa kuingia katika bodi ya MCT ni Usu mallya,Prof.Ruth Meena na jaji Thomas Mihayo .

WaWakati huo huo wajumbe wa baraza la habari Tanzania (MCT) wamelalamikia hatua ya vituo vya radio za masafa mafupi nchini kujikita zaidi katika kushambuliana na kutumia lugha za matusi badala ya kutimiza misingi ya uanzishwaji wa chombo hicho kwa mujibu wa leseni zao zilizotolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).

Wajumbe hao wametoa malalamiko hayo katika mkutano mkuu wa 14 wa MCT uliomalizika katika ukumbi wa Hotel ya Lion iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam na kuliomba baraza la habari Tanzani kuvibana vituo hivyo vya radio ambavyo vinakwenda kinyume na taaluma ya tasnia ya habari hapa nchini.

Mjumbe Abubakar Karsaani na Greyson Mgoi ambaye ni mwalimu wa chuo cha Times School Of Journalism (TSJ) Ilala alisema kuwa hivi sasa vituo vya radio vya masafa mafupi ambavyo vimeendelea kuanzishwa katika mikoa mbali mbali mbali ya kukuza suala zima la utandawazi na ukuaji wa tasnia ya habari kwa umma ila bado baadhi ya vyombo hivyo vimekuwa vikiendeshwa pasipo kufuata maadili ya Tasnia hiyo kutokana na kutumika kutukana watu na kwa vile vya dini pia vimekuwa vikitumika kushambulia dini nyingine .

“ Siku za hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia lugha zisizo nzuri ambazo zimekuwa zikitolewa na Radio hizi ….ni vizuri sasa baraza la habari kuangalia jinsi ya kuzifanya radio hizi kufuata maadili ya utangazaji ili kulinda heshima ya tasnia hii hapa nchini”

Mjumbe Mgoi alitaka radio kuacha kuendelea kuwatumia watangazaji wa vipaji na badala yake kuzingatia sifa zinazohitajika wakiwemo waliopata mafunzo ya uandishi wa habari .

Hata hivhyo wajumbe wa mkutano huo walitaka MCT kuwabana wanachama wake ambao wanashindwa kulipa ada kwa wakati kama njia ya kukifanya chama hicho kuwa endelevu zaidi na chenye wanachama hai.

Mjumbe Keneth Simbaya ambaye ni Rais pia wa muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) alisema kuwa ili MCT iweze kufanya vizuri zaidi ni pamoja na wanachama wake kupenda kulipa ada na kukipenda chama chao.

Alisema kuwa hata wahisani mbali mbali wanaotaka kuisaidia MCT kutoka nje ya Tanzania kwanza wamekuwa wakitaka kujua jinsi ambavyo wanachama wa MCT wanavyojibidiisha kwa ajili ya kukiendesha chama hicho na kuwa suala la wanachama kulipa ada linapaswa kutiliwa mkazo zaidi.

Kwa upande wake katibu mtendaji wa MCT Kajubi Mkajanga akizungumzia suala hilo alisema kuwa bado vyombo hivyo vya habari vinapaswa kufuatia maadili ya habari na kuwa MCT pamoja na TCRA na Vilabu vya waandishi wa habari mikoani vitaendelea kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha kuwa maadili na taaluma ya habari yanazkingatiwa.

Akielezea juu yamkutano huo Mkajange alisema kuwa moja kati ya mambo yaliyojadilkiwa katika mkutano huo ni pamoja na kufanya marekebisho ya katiba ,kufanya marekebisho ya viwango vya ada kwa wanachama wake pamoja na kuchangua bodi mpya baada ya ile inayoongozwa na jaja Kisanga kumaliza muda wake.

Mmoja kati ya wajumbe wa Baraza hilo, Mshana, ambaye pia ni Mkurgenzi Mtendaji wa Magazeti ya The Guardian Ltd, akipiga kura.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.