Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KUFUNGUA MAONYESHO YA 35 YA KIMATAIFA YA BIASHARA KESHO

Mwenyekiti wa mfuko furusasawa kwa wote (EOTF) Mama Anna Mkapa (kulia) akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na Kampuni ya  Camphill Handlouly Weavers wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya 35 ya biashara ya Kimataifa, yanayotarajia kufunguliwa rasmi kesho na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal,  yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Irene Lomanyani.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Alzin Matuy, akipewa maelekezo ya huduma ya Internet kutoka kwa wataalamu wa simu za mkononi wa kampuni  Daudi Dominick (kulia) na Mwita John.wakati alipotembelea banda hilo katika maonyesho ya Kimataifa ya 35 yanayoendelea katika Viwanjavya sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.