KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, leo amekutana na wamiliki wa Blogs za Bongo na kubadilishana mawazo ikiwa ni sehemu ya kuboresha njia ya mawasiliano kupitia mtandao na hasa Blogs.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Nape alisema kuwa anazipongeza Blog zote kwa kuwa mstari wa mbele katia kuwafikishia ujumbe na habari kamili kwa wakati wananchi na kwamba amekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia habari zinazotolewa kupitia blogs.
“Kwa upande wangu mimi ninakawaida ya kupitia Blogs zote kila asubuhi na jioni kabla ya kulala na kujionea mambo ambayo huenda siku ya pili naweza nisiyapate katika magazeti, kwa kweli nawapongeza sana kwa kazi zenu,
Na hili si kwa chama cha CCM pekee bali pia hata Serikali inatambua uwepo wenu na ndiyo maana mmekuwa mkitambulika kwa haraka zaidi na kufuatiliwa kila habari mnazozitoa katika blogs zenu” alisema Nape
Aidha nape aliwataka Mablogger kuendelea na jitihada za kuwahabarisha wananchi na kuwapa hata yale ya kuwarekebisha viongozi pale wanapoonekana kuzembea katika kazi zao.
Alitolea mfano wa Jengo la Sukita kuwa ni ndipo kilipoanzia Chuo Kikuu cha Dar es salaam, ambacho kwa sasa kimeshapiga hatua kubwa, lakini kuna watu bado hadi leo hii hawajui historia hiyo, hivyo kupitia Blogs wanaweza kufanya habari za uchunguzi na kuwaonyesha wananchi utofauti wa histotia kama hizo.
Nape pia aliwataka wanablogs hao kuwa naumoja wao yaani Chama cha Mablogger, jambo ambalo ajibiwa kuwa tayari ni watu wanaofanya kazi zao chini ya Ngao, na kuowaomba kutoa ushirikiano katika maandaliazi kuelekea sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, ili watu waweze kuona utofauti kati ya Enzi za Tano na CCM ya sasa.
“Lakini pia tumeanza maandalizi ya sherehe za kuzaliwa Chama cha Tano ambazo zitafanyika Julai 7 mwaka huu, kwa ajili ya kuwakumbusha wananchi chama chetu kilipoanzia” alisema Nape.
Aidha alisema kuwa CCM imeamua kukivunja Kitengo cha Propaganda na kuunga Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma ili kuweza kutoa na kupata taarifa kwa haraka na wakati.
Nape, akipozi kwa picha na baadhi ya wanablogger, baada ya kikao hicho. Kutoka (kushoto) ni Anthony Siame-Siamepix.Blogspot.com, Zainul Mzige-Mo Dewj Blog, Shamim Mwasha-8020 Fashion Blog, Mroki Mroki-Mrokim.blogspot,Nape Nnauye, katibu NEC, Muhidini Sufiani-Sufianimafoto.blogspot.com, ambaye ni mmiliki wa blog hii,Mtoto wa Kitaa.blogspot, Rajab Mhamila-Burudani mwanzomwisho.blog,Francis Dande, mwakilishi wa Michuzi Blog,Jofrey Mwakibete, mpigapicha wa Mo Dewj Blog, Othman Michuzi-Mtaa kwa Mtaa blog na Dj Choka-Dj Choka Blog.
No comments:
Post a Comment