MABINGWA wa soka Tanzania Bara msimu uliopita wa 2010 Simba ya jijini Dar es Salaam, kesho wanatarajia kujitupa uwanjani kufungua Dimba la michuano ya Kombe la Kagame, ambapo watavana na timu ya Vital O' ya Burundi, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba kama wenyeji wa michuano hiyo watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Warundi hao ambao nao wamekuja kutaka kuweka heshima na historia katika Soka la Afrika kutokana na kutopata nafasi ya kufika fainali ya michuano hiyo ya kila mwaka.
Mchezo huo utaanza saa 10 Alasiri huku mchezo wa kwanza utakuwa saa 8.00 mchana ambao utakuwa ni kati ya Etincelles ya Rwanda na Zanzibar Ocean View ya Zanzibar, mechi zote zikiwa za kundi A.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mchana Katibu Mkuu wa
Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicolaus Musonye, alisema kuwa maandalizi ya michuano hiyo yanaendelea kama yalivyopangwa na
wenyeji Simba wataanza kufungua mashindano hayo dhidi ya Vital O.
Alisema mechi za siku ya pili yaani Jumapili ni za kundi B na kundi C, ambazo nazo
zitakuwepo kama zilivyopangwa.
Aidha Musonye, alisema Jumapili katika Uwanja wa Taifa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2011, Dar Young Africans ya Jijini Dar es Salaam,itachuana na El Mereikh na mchezo mwingine utakuwa ni kati ya APR ya Burundi dhidi ya Ports, na katika kundi C St George dhidi ya Ulinzi mchezo utakaofanyika jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Musonye alisema kundi A limeongezeka ambapo sasa litakuwa na timu tano na timu tatu zitaingia katika hatua ya robo fainali wakati makundi yaliyosalia kila moja
litatoa timu mbili.
Aliyataja makundi hayo kuwa ni:- Kundi A ni timu za Vital O, Etincelles ya Rwanda na Zanzibar Ocean View ya Zanzibar na Red Sea ya Elitrea.
Kundi B ni timu za Yanga ya Tanzania, El Mereikh ya
Sudan, Bunamwaya ya Uganda na Elman FC ya Somaria,
Kundi C, limebeba timu za APR ya Rwanda, St
George ya Ethopia, Ulinzi ya Kenya na Ports ya Djibut.
Zaidi ya timu nane zinazoshiriki mashindano hayo tayari
Zimekwishawasili nchini.
No comments:
Post a Comment