Habari za Punde

*HATA MAJUU WAPO KAMA BONGO

 Mtoto akipita katikati ya foleni ya magari na biashara yake akitafuta wateja wa kununua vijidoli vya watoto, hii si kwa Bongo pekee bali hata katika mataifa yaliyoendelea kumbe wapo. Hapa ni katika moja ya Barabara ya Jiji la Istanbul Uturuki.
 Mandhari kama hii si rahisi kuikuta katika mitaa yeyote ya Bongo bali ni kwa watu wenye uelewa pekee ambao hata kipisi cha sigara tu huona kero kukitupa barabarani bali hujali zaidi na kutupa katika vifaa vilivyo maalum kwa ajili ya takataka pembezoni mwa Barabara. Je ni lini sasa Wabongo tutaelimika kuhusu usafi wa Mazingira?
Na hii ni kwa wenzetu pekee ambao hata waenda kwa miguu hufuata sheria za usalama Barabarani, kwani hata kama hakuna gari linalopita kwa wakati huo wao husimama na kusubiri kuruhusiwa na taa za kuingozea magari na watu hadi ziruhusu. Hapa wakisubiri kuruhusiwa na taa katika moja ya barabara ya Istanbul Uturuki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.