Habari za Punde

*JAKAYA AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUMBUKUMBU YA KUWAENZI MASHUJAA WETU

Askari walikuwa wakikusanyika kwa kusikia mlio wa King'ora hiki cha
kuzungusha kwa mkono.
 BEATRICE MLYANSI  NA  JOSEPH ISHENGOMA, MAELEZO-MTWARA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu  Dkt. Jakaya  Mrisho  Kikwete jana aliwaongoza mamia ya wananchi katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa iliyofanyika  kitaifa katika makaburi ya mashujaa Naliendele mkoani Mtwara.
Baada ya kuwasili katika makaburi hayo ya mashujaa, Mhe.rais aliweka silaha za asili ambazo ni mkuki na ngao katika mnara wa kumbukumbu za mashujaa.
Mzee Ernest Waya, mkazi wa mkoani Mbeya akiweka upinde na mshale katika Mnara wa mashujaa uliopo mkoani Mbeya, kuwakumbuka wapiganaji wenzake aliokuanao katika Vita Kuu ya pili ya Dunia. Ernest , ameitaka Serikali kuwakumbuka wazee hao na si kukumbukwa siku ya maadhimisho hayo pekee ambayo hufanyika mwaka hadi mwaka.
Kifaa cha Mawasiliano kilichokuwa kikitumiwa na askari wetu.
Aidha mkuu wa majeshi ya Usalama na Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange aliweka sime, Kiongozi  wa Mabalozi nchini Balozi Juma Alfani Mpango aliweka shada  la maua,wakati Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Selemani Mtalika Shiringi aliweka upinde na mishale na Kiongozi wa Tanzania Legion Ezekiel Chacha aliweka shoka.
Kisha viongozi wa dini wakiongozwa na Sheikh Jamaldin Salim Chamwi alisoma dua kwa niaba ya Waislamu ,Mchungaji Lucas Mbedule alisoma sala kwa niaba ya Jumuiya ya Wakristu Tanzania na Mhasham Askofu Gabriel  Mmola alisoma sala kwa niaba ya Wakatoliki.
Baada ya sala hizo Mhe.Rais alitembelea makaburi na kisha kuwasalimia wananchi na kuwashukuru wananchi kwa kufika katika sherehe hizo muhimu kitaifa na kusema “Lengo la Sherehe hizi ni kusherehekea maisha ya mashujaa sio kufa kwao.”
“ Lengo la sherehe hizi ni kusherehekea maisha ya mashujaa sio kufa kwao,.Mashujaa hawa walilipa gharama kubwa kwa kutoa uhai wao kwa nchi yao”alisema Rais Kikwete.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Eng.Felipe Jacinto Nyusi alitoa shukrani kwa Tanzania kwa niaba ya nchi yake jinsi ilivyosaidia kuleta amani na utulivu nchini mwake.
“Nawashukuru  sana watanzania maana uhuru wetu umetoka hapa,sasa tumetulia nyumbani kwa sababu ya damu iliyotulia hapa Naliendele.”alisema  Waziri Nyusi.
Moja ya silaha iliyotumiwa na askari wetu katika kutafuta Ukombozi
wa watu wa Msumbiji
Viongozi wengine wa kitaifa waliohudhuria maadhimisho hayo ni makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal ,Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali.
Sherehe hizi ni za pili kufanyika nje ya jijini  la Dar es salaam ambapo mwaka 2009 zilifanyika katika makaburi ya Kaboya mkoani Kagera.
Hili ni moja kati ya Majeneza yaliyotumika kubebeba masalia ya Miili ya askari wetu na kuwasafirisha kutoka Msumbiji kuja Tanzania

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.