Habari za Punde

*JUMUIYA YA WANAMITANDAO YAMPA BIG UP J. MMBANDO KWA KUHAMIA


Jumuiya ya wanamitandao ya jamii (Social networks) nchini inachukua nafasi ya hii kumpongeza mwanahabari mwenzetu, Jackson Mmbando, (pichani kushoto akigawa misaada siku yake ya kwanza kazini Jumatatu ya jana)  kwa kupata nafasi ya kupiga mzigo Airtel Tanzania kama bosi wa Mahusiano wa kampuni hiyo ya simu za mikononi.

"HONGERA KWA KUHAMIA" Jumjuiya inakutakia kazi njema na endeleza mahusiano yako mazuri na vyombo vyote vya habari ambavyo umekuwa ukifanya navyo kazi kwa ufanisi toka huko ulikotoka, na ambako pengo lako halitozibika kirahisi. 

Waswahili walinena, "myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni".  

Kaka kazi unaiweza! Kila la kheri wewe na familia yako mpya ya Airtel Jumuiya ya wanamitandao

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.