Habari za Punde

*YANGA KUANZA KAMBI YA MAANDALIZI YA LIGI KUU KESHO


MABINGWA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mabingwa kombe la Kagame,  Yanga ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kuinaingia kambini kesho kwa ajili kuanza maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao unaotarajia kunza Agosti 20 mwaka huu.

Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu Ofisa Habari wa yanga Louis sendeu alisema Uongozi wa Klabu hiyo unajitahidi kujaribu kuanzaa mchakato wa kuandaa mchezo wa  kirafiki wakati wakia kambini iwapo itapatikana timu kali na yenye uwezo ili kuwapa mazoezi.


Aidha Sendeu alisema kuwa baada ya mchezo wa kujipima nguvu iwapo utakuwepo basi Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu watacheza mechi ya kuwania Ngao ya hisani dhidi ya Simba, mchezo utakaochezwa Agosti 13 kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo bado Ngao hiyo ya Hisani bado iko mikononi mwa Mabingwa hao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.