Habari za Punde

*MDAU GUNDUA UTOFAUTI WA HIZI BENDERA JAPO ZOTE ZINAMAANISHA NI BENDERA YA TANZANIA

 Kwa umakini Bendera hii kama ambavyo tumekuwa tukifundishwa toka elimu ya msingi maana halisi ya rangi zinazobeba na kuitambulisha bendera ya Tanzania ni kama rangi hizi zinavyoonyesha sawa. 
Lakini ukiangalia kwa makini endapo utakuwa nje ya nchi na ukakuta Bendera yenyemapugufu bila kujua unaweza kuikana bendera yako bila wewe kujua wala kujitambua kwani utofauti wa bendera hizi ni mkubwa na sijui ipi ndoyo yenye rangi sahihi inayotakiwa kumaanisha kile inachokimaanisha. 
Rangi ya Bluu kwa kawaida huwakilisha Bahari na ndiyo maana katika bendera upande wenye rangi ya Bluu huwa na rangi ya Bluu Bahari, tofauti na rangi hii inayoonyesha kukorea zaidi na kupoteza maana na uhalisia wa rangi yenyewe. 
Hivyo hivyo na katika Bendera hii pia rangi ya Kijani kwa kawaida humaanisha misitu ama uoto wa asili, hivyo rangi yake nadhani hutakiwa kuwa ni yakijani iliyokorea zaidi kama ilivyo ya juu, sasa sijui kama inaingia akilini kubadilisha rangi ya bendera ya Taifa ama hali yakuwa unaelewa endapo utabadili rangi basi umepoteza maana na halisi ya utaifa ni sawa na kuongeza manjonjo katika ukimba Wimbo wa Taifa. 
Je ulishwahi kusiki msanii akatoa Wimbo wa remix wa Wimbo wa Taifa??? Haiwezekani basi ndivyo isiwezekane hata katika alama nyingine za Taifa ikiwamo Bendera ambayo ni nahisi ni alama kubwa ya kwanza kati ya alama tano za Taifa letu la Tanzania. Mungu Ibariki Tanzania Amen!!!!. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.