Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAONYESHO YA 35 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua rasmi maonyesho ya 35 ya Biashara  ya Kimataifa , wakati alipotembeleea maonyesho hayo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam, leo.
 
  Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF, wakifurahia kwa pamoja na tuzo yao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimabidhi Tuzo ya ushindi wa jumla Mkurugenzi Mkuu NSSF, Dkt Ramadhan Dau, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Bunge, Owen, wakati alipotembelea Banda la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere alipofika kuzindua rasmi maonyesho ya 35b ya Biashara ya Kimataifa.
 Akiendelea kutembelea na kukagua mabanda, hapa ni wakati akitoka kukagua Banda la Home Shopping Centre.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Imani Kajula, wakati alipotembelea na kukagua Banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa, baada ya Makamu kuzinduz maonyesho hayo rasmi leo . Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Mark Wiessinga.
 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akitoa burudani mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzizi wa maonyesho hayo.

Mwakilishi wa SBL, akiwa na tuzo yake baada ya kukabidhiwa kama wadhamini wakuu wa kinywaji cha maonyesho hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.