Habari za Punde

*MAPACHA WA3 WAIPA BIG UP EXTRA BONGO

 Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki (kushoto) akiimba jukwaani na mwimbaji wa bendi mpya ya Mapacha wa3, Kalala Junior, wakati wa onyesho la bendi ya extra bongo lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa  Zonghwaa Victoria jijini Dar es Salaam. 

Kalala aliyeongozana na wanamuziki wenzake wa Mapacha wa3, Khalid Chokoraa na Jose Mara, walipanda jukwaani na kuimba sehemu ya vipande vya muziki wa Extra Bongo na kuwapagawisha mashabiki wa bendi hiyo vilivyo huku wakichomekea sehemu ya vipande vya miondoko ya baadhi ya nyimbo zao jambo lililowafanya kushangiliwa na kutunzwa na watu lukuki. 

Wakizungumza na Michael Machellah Reporter wa mtandao huu, baada ya onyesho hilo, wanamuziki hao walisema kuwa wanatambua uwezo wa kaka yao Ally Choko kuwa si wa kubahatisha kutokana na kuwa hata wao ni sehemu ya matunda ya Mkurugenzi huyo wa Extra Bongo kutokana na kuwaibua kama Chokoraa Fergaso na wengineo ambao wanaona soo kusema ukweli.
 "Lakini kwa upande wetu sisi tunamkubali vilivyo na kumuheshimu kama kaka yetu na mkubwa wetu katika jukwaa hili la muziki wa dansi na tutaendelea kumuunga mkono na hata kumpa sapoti pale atakapotuhitaji kwa jambo lolote" alisema Chokoraa.
Ally Choki, akishambulia jukwaa na Khalid Chokoraa wa bendi ya Mapacha wa3. Chokoraa ni mmoja kati ya wanamuziki wanaoendelea kufanya vizuri katika jukwa la muziki wa dansi ambaye pia ni mmoja kati ya wanamuziki walioibiliwa na Ally Choki

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.