Habari za Punde

*FOLENI YA DAR ITAISHA LINI????

Kwa mtazamo wangu kuhusiana na foleni inayozidi kushika kasi kila kukicha itakuwa ni ndoto za lenacha kuisha kwa karne hii tuliyonayo kutokana na kwamba kila kukicha magari yanazidi kuongezeka na miundombinu yetu ni ile ile isiyobadilika kuendana na ongezeko la magari. 

Hii ni Barabara ya Nyerere eneo la Tazara likiwa na foleni ambayo ni kawaida kwa kila siku kuwepo mida ya saa za asubuhi na jioni na tatizo hili si kwa eneo hili tu pekee bali ni karibu katiki maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam, muda umefika sasa wa wizara husika kuboresha miundombinu ili kuweza kuendana na ongezeko la magari yanayodi kila kukicha jijini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.