Habari za Punde

*MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHAA KUFANYIKA LEO UKUMBI WA PANANDI PANANDI ILALA

Mdau wa michezo Amir Mohamedi 'Msauzi' akimkabidhi maji kwa niaba ya mdau Prince Muddy Kalla wa Ilala kwa Kocha wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' katoni 15 za maji kwa ajili ya mashindano ya kuhamasisha mchezo wa ngumi itakayofanyika leo jumapili. Picha na Mpigapicha Wetu
***********************************

Mapambano hayo ya raundi nne, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa
Panandi Panandi uliopo bungoni Wilaya ya ILala ambapo mabondia wanne
kutoka katika kila klabu, watachapana makonde leo katika mapambano yasiyokuwa ya ubingwa..

Mabondia wa Amana watakaopanda siku hiyo ni IBrahimu Class Kg.64,
Khalfani Othumani Kg 57, Kassimu Sambo Kg 54, na Saidi Ally Kg 48.
Klabu ya Matimbwa itawakilishwa na MOhamedi Matimbwa Kg 64, MOhamedi
Muhani Kg 57, Edson Joviki Kg 54 na MOhamedi Kumbilambali Kg 48 na Klabu ya Ashanti ni Uwesu Manyota,Ramadhani Kimangale,Mark Edson

Akizungumza Dar es Salaam leo Mratibu wa mapambano hayo ambae pia ni
kocha wa mchezo wa ngumi akishirikiana na Kinyogoli Foundition, Rajabu

Mhamila Super D, Alisema mpango huo utaendelea mpaka wahakikishe
wamefanikiwa kuibua vibaji na kuviendeleza

Alisema tangu waanze mpango wa kuandaa mapambano mkohani humo
wamefanikiwa kurudisha hamasa ya mchezo huo mkoani humo na kuwataka
wadau mbalimbali kutoa sapoti kwa mchezo huo ili upate kuendelea
ambapo Super D alitoa mfano wa vitu wanavyoviitaji ikiwemo posho za
nauli kwa wachezaji vifaa vya kuwatia moyo na zawadi mbalimbali kwa
mabondia

Super D aliwashukulu wadau waliojitolea katoni 15 za maji kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo yatakayofanyika jumapili ya Julai 17 aliwataja waliosaidia kuwa Mohamed Sadiq 'Muddy Kala' na Mwanamama Halima Kaubanika aliyejitolea maji kwa wachezaji wote watakaocheza kwa siku hiyo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.