Waendesha Pikipiki, Adil Othman (mbele) akichuana na Ludan Volvo, wakati wa mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Adil ni mtaalam wa kutumia Pikipiki yenye matairi manne aina ya Quad Bike na Volvo ni mtaalam katika pikipiki ya matairi mawili, hapa wakionyeshana ujuzi.
Na Sufianimafoto, Reporter jijini Dar
Mchezo huu ni mchezo unaovutia na wenye mvuto mkubwa kwa watu waliowengi pale wachezaji wa mchezo huu wanapoamua kuanza kufanya manjonjo, yaani kuonyesha maujuzi ya kuchezea vyombo hivi vya moto na kuwakusanya watu hata wasiotarajiwa na kujizolewa mashabiki lukuki kwa dakika chache tu.
Lakini cha kushangaza hadi hii leo mchezo huu bado unakimbiwa na wadhamini na kila anayedokezwa kuhusu kudhamini mchezo huu bado anakuwa na roho ya kusita sasa sijui ni kwamba wengi wanakuwa hawaujui mchezo huu ama wengi wanaona ni mchezo wa kutisha, lakini yote kwa yote bado ni mchezo kama ilivyo michezo mingine na hivyo ina kila sababu za kusaidiwa kupiga hatua kama ambavyo nchi jiraji wameweza kuuendeleza mchezo huu hadi hatua za kimataifa, kama vile Uganda na Kenya.
Makampuni mengi yamekuwa yakidhamini michezo mingine kama Soka, Urembo na mingineyo na kuusahau mchezo huu ambao ipo siku utakuja kuwa ni mchezo bora na wenye kuiletea sifa nchi hii kimataifa iwapo watajitokeza watu wenye uwezo na kuusimamia ipasavyo mchezo huu.
Kwa sasa wachezaji wengi wa Bongo wa mchezo huu wamekuwa wakijitolea zaidi na kucheza kama njia mojawapo ya kujifurahisha tu bila kuwa na malengo, japo kuna wakati wao kama wao wamekuwa wakijitahidi kujipenyeza na kutafuta mechi za mialiko ya kimataifa na baadhi yao wamekuwa wakienda kushiriki na kufanya vizuri, lakini bado wamekuwa wakirudi kimya kimya na kutulia na hii yote ni kwa sababu wanakuwa hawana muongozo wa kutosha na wahana sapoti ya kutosha.
Ni wakati sasa wa baraza la michezo kuuangalia mchezo huu kwa jicho la pili na kuuinua kama ilivyo michezo mingine ili tuweze kujivunia, kwani wachezaji wazuri wa mchezo huu tunao wa kutosha ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam.
Tayarui wachezaji hawa wamekwisha unda umoja wao na kuwa na chama kinachotarajia kutambulika kiserikali hii ni hatua moja ambayo inatakiwa msaada ili mchezo huu kuweza kuwa katika ramani kama ulivyo katika nchi nyingie Duniani.
Mwendesha Pikipiki wa Kambi ya Kinondoni, Ludan Volvo, akionyesha mbwembwe za kutembea na tairi moja wakati wachezaji wa mchezo huo walipokuwa katika mazoezi ya kawaida ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waendesha Pikipiki wakianza mwendo kwa pamoja wakati wakishindana katika mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwendesha Pikipiki, Adbul, akiwa hewani baada ya kuruka Tuta.
Mwendesha Pikipiki, Adil Othuman, akionyesha uwezo wa kuitumia pikipiki ya matairi manee aina ya Quad Bike, wakati wa mazoezi ya waendesha pikipiki hao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Waendesha Pikipiki wakianza mwendo kwa pamoja wakati wakishindana katika mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwendesha Pikipiki, Adil Othuman, akionyesha uwezo wa kuitumia pikipiki ya matairi manee aina ya Quad Bike.
Waendesha Pikipiki, Dotto Juma (mbele) akichuana na Ludan Volvo, wakati wa mazoezi yao ya kujiweka fiti yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment