KOCHA wa mchezo wa ngumi za Ridhaa Rajab Mhamila 'Super D' katika kuendeleza mchezo wa ngumi za Ridhaa Katika Mkoa wa
Kimichezo wa ILALA, ameandaa mapambano yatakayozikutanisha timu za Amana, Matimbwa,Ashanti,Bigrayt na klabu nyingine, Julai 17 mwaka huu.Mapambano hayo ya raundi nne, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi, uliopo bungoni Wilaya ya ILala ambapo mabondia wanne kutoka katika kila klabu, watapambana.
Mabondia wa Amana watakaopanda ulingoni siku hiyo ni, Ibrahim Class, Kg.64, Khalfani Othumani Kg 57, Kassimu Sambo Kg 54, na Saidi Ally Kg 48.
Klabu ya Matimbwa itawakilishwa na Mohamedi Matimbwa Kg 64, Mohamed Muhani Kg 57, Edson Joviki Kg 54 na Mohamed Kumbilambali Kg 48.
Na Klabu ya Ashanti ni Uwesu Manyota,Ramadhani Kimangale na Mark Edson.
Akizungumza na Sufianimafoto jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mapambano hayo, Rajab Mhamila ambaye pia ni kocha wa mchezo wa ngumi akishirikiana na Kinyogoli Foundition, alisema mpango huo unalengo la kusaka na kuibua vipaji na kuviendeleza.
Aidha alisema kuwa tangu kuanza kwa mpango huo wa kuandaa mapambano mkoani wa Dar umefanikiwa kurudisha hamasa ya mchezo huo na kuwaomba wadau wadau mbalimbali kutoa sapoti kwa mchezo huo ili waweze kusonga mbele
No comments:
Post a Comment