Habari za Punde

* PASCAL ISSA KUFANYIWA UPASUAJI JUMATATU KATIKA HOSPITALI YA CCBRT

Kijana Pascal Issa ambaye amefanikiwa kupata msaada wa upasuaji wa kuondoa mfupa wa ziada akiwa katika Hospitali ya CCBRT kufuatilia taratibu za upasuaji huo utakaofanyika Jumatatu kwa msaada wa Bw. Salum Awadhi na Hospitali ya CCBRT ambayo imetoahuduma ya Malazi na Chakula mpaka atakapopona katika Hospitali hiyo. Kulia kwake ni Mpiga picha wa MO BLOG Geofrey Mwakibete wakifurahia jambo.
***************************************


Msaada huo uliotolewa na Bw. SALUM AWADHI kwa Kijana PASCAL umekuja baada ya kijana huyo kufika kwenye ofisi za Mo Blog Kwenye jengo la PPF TOWER Jijini Dar Es Salaam kuomba wasamaria wema kumsaidia kupata matitabu ya mguu wake huo ambao umemtesa kwa miaka 17.
Moblog inapenda kuchukua fursa hii ya kipekee kumshukuru kwa Dhati Bw.SALUM AWADH kwa moyo wake wa ukarimu kwa kukubali kugharimia matibabu ya kijana huyu pamoja na Hospitali ya CCBRT kwa msaada wao sambasamba na wadau wengine walioguswa kwa njia moja ama nyingine lakini hawakuwa na uwezo wa kusaidia moja kwa moja pamoja na Wana Blog wote waliosaidia kutoa taarifa ya kijana huyu.
MO BLOG itaendelea kuwaletea taarifa za maendeleo ya Pascal Ambaye anatarajiwa kulazwa siku ya Jumapili kwaajili ya maandalizi ya Upasuaji wa kuondoa mfupa huo wa Pili .
MO BLOG pia inawakaribisha wale ambao wako tayari kumsaidia kijana huyu kuuguza kidonda baada ya upasuaji waendelee kuwasiliana kupitia namba hizi. +255714940992 na +255657069870.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.