Waandamanaji katika mji wa Hama
Syria imeishtumu Marekani kwa "kuingilia" masuala yao ya ndani baada ya balozi wa Marekani nchini humo kusafiri hadi katika eneo la machafuko la mji wa Hama.
Wizara ya mambo ya nje ya Syria inasema ziara hiyo ya Robert Ford ilikuwa "ushahidi wazi" kuwa Marekani inahusika na maandamano yanayoendelea nchini humo.
Mapema, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kuwa ziara ya Bwana Ford ilikuwa ni kuwaunga mkono waandamanaji.
Mamia ya wakaazi wa Hama wamekimbia wakiogopa kushambuliwa na vikosi vya usalama.
Vifaru vya kijeshi vimewekwa nje ya mji na takriban watu 22 wameuawa katika siku za hivi karibuni.
Serikali ya Marekani inasema kuwa Bwana Ford anatarajiwa kubaki Hama kwa ajili ya maandamano dhidi ya serikali ambayo kwa kawaida hufanyika baada ya sala ya Ijumaa.
Mwandishi wa BBC Kim Ghattas mjini Washington amesema kuwepo kwa balozi wa Marekani mjini Hama kunaweza kumkamfanya Rais wa Syria Bashar al-Assad kushindwa kufanya mashambulio makali eneo hilo.
Lakini hatua hiyo imekera sana serikali ya Syria.
Maandamano
" Kuwepo kwa balozi wa Marekani mjini Hama bila ruhusa ni dhihirisho wazi la matukio ya hivo karibuni,na jaribio lao la kutaka kuzidisha machafuko, ambayo yanaharibu usalama na amani ya Syria," wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa.
Maandamano ya Ijumaa iliopita mjini Hama yalikuwa moja ya maandamano makubwa katika muda wa miezi mitatu kuwahi kufanyika nchini Syria.
Siku moja baadaye, Bwana Assad alimfuta kazi gavana wa eneo hilo Ahmad Khaled Abdel Aziz kwa kushindwa kukabiliana na maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment