Habari za Punde

*TETESI, SIMBA KUWAREJESHA PAWASA, MACHUPA NA COSTA?

Habari kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu kabisa na Naniliu wa Klabu ya Simba umetonya kuwa baada ya kuwatupia virago mshambuliaji, Mussa Hassan Mgosi na kiungo, Mohamed Banka pamoja na uhakika wa kumnasa Sunzu lakini bado wamedhamiria kirejesha kikosi cha zamani cha timu hiyo kilichopata kutamba katika safu ya ulinzi na ushambuliaji, yaani Pawasa na Costa pamoja na kufanya jitihada za kumrudisha machupa ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
"Unajua hii ilishapangwa tangu awali na mipango inaendelea na ilitakiwa tuwe tumekalisha kabla ya kumalizika kwa usajili wa dirisha dogo, na pia hawa unaowasoma leo katika magazeti walishaachwa tangu awali ila ni Kocha tu aliwahitaji kwa ajili ya michuano ya Kagame na endapo Simba ingefungwa katika hatua ya nusu fainali basi kesho yake tu baada ya mchezo huo ilipangwa kutangazwa rasmi kuachwa kwa wachezaji hao na wengine kuuzwa kwa mkopo katika Klabu za Moro United na nyinginezo." alisema mtonyaji huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe mtandaoni humu. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.