Habari za Punde

*WAZIRI MEMBE KESHO KUWA MGENI RASMI SHINDANO LA MISS VYUO VIKUU HURIA KINONDONI


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe atakuwa mgeni rasmi katika mashindano ya urembo ya kumsaka mrembo wa Chuo Kikuu Huria yaliyopangwa kufanyika kesho Ijumaa jioni kwenye ukumbi wa chuoni hapo Kinondoni.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 11 kutoka matawi mbali mbali ya chuo kikuu huria kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano, Albert Memba.

Memba alisema kuwa Waziri Membe amethibitisha kuwepo kaika mashindano hao ambayo yatapambwa na bendi ya Mapacha Watatu na msanii wa bongo fleva, Lina.

Aliwataja warembo ambao watachuana leo kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Miss Tanzania kuwa ni Grace Dominic, Weirungu David, Bella Edward, Nemesia Simon, Jemima Maole, Magdalena Assey, Neema Mtitu, Sophia Chacha na Valentine Uwonga.

Warembo hao walikuwa kambini hotel ya Chichi iliyopo Kinondoni chini ya mkufunzi wao ambaye ni miss chuo kikuu huria wa mwaka 2009, Shine Mkali.

“Tunatarajia kuwa na shindano kali ambalo litatao warembo bora ambao tunaamini watashinda katika mashindano ya Vodacom Miss Tanzania mwaka huu na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia, Miss World,” alisema Memba.

Washindi watatu wa mashindano hayo watapata fursa ya kupambana katika mashindano ya Miss Tanzania yaliyopangwa kufanyika baadaye

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.