Habari za Punde

*TWIGA STARS KUKIPIGA KESHO KUSAKA MEDALI YA SHABA YA MSINDI WA 3

TIMU ya Soka ya Wanawake (Twiga Stars) inaingia tena uwanjani kesho kusaka medali ya shaba (mshindi wa tatu) katika michuano ya COSAFA kwa kupambana na Malawi katika mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Rufaro hapa Harare.
Leo asubuhi timu hiyo imefanya mazoezi na jioni itapumzika tayari kwa mchezo huo
utakaoanza saa 6.30 mchana kwa saa hapa ambapo nyumbani ni saa 7.30 mchana.
Katika Jiji la Harare hivi sasa ni kipindi cha baridi kwa siku nzima.
Twiga Stars ambayo leo imealikwa kwa Balozi kwa ajili ya chakula cha jioni
itarejea nyumbani Jumatatu saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Baadaye
saa 5 kamili asubuhi wachezaji na kocha Charles Mkwasa watakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika ofisi za TFF.
Boniface Wambura
TFF Media Officer
Harare

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.