Habari za Punde

*YANGA USO KWA USO NA SIMBA FAINALI YA KOMBE LA KAGAME NAYO YAPITA KWA MATUTA

 Kikosi cha kwanza cha Yanga kulichoanza mtanange wa leo.
 Godfrey Taita wa Yanga (kushoto) akichuana kuwania mpia na Beki wa St. George ya Ethiopia, Abebaw Butako, wakati wa mchezo wa Fainali za Kombe la Kagame uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Yanga imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali hizo baada ya kuwagalagaza St. George kwa mikwaju ya Penati 5-4. Picha na Blog ya Michuzi
Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa timu hizo bila kufungana na hatimaye kuongezwa dakika 30 ambazo pia zilimalizika bila kupatikana mbabe jambo lililopelekea timu hizo kuingia kwenye hatua ya kupigiana mikwaju. 
Kwa hatu hiyo sasa Yanga itakutana na watani wake wa Jadi Simba ambao nao pia jana walifanikiwa kutinga katika fainali hizo kwa njia ya mikwaju ya penati, St. George sasa itavaana na El-Mereikh ya Sudan katika kusaka mshindi wa tatu wa michuano hiyo mchezo unaotarajia kupigwa keshokutwa jumapili mchana kwenye uwanja wa Taifa kabla ya mchezo wa fainali wa Watani hao wa jadi utakaochezwa siku hiyo hiyo.
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi huo wa timu yao baada ya kuibika na ushindi wa penati 5-4.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia huku wakiwa na bango linalowakebehi watani wao wa Jadi Simba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.