Habari za Punde

*WAAMUZI 14 WAPATA BEJI ZA FIFA

JUMLA ya Waamuzi 14 wakiwemo wawili wapya wamefanikiwa kupata beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2012 baada ya kufaulu mtihani wa waamuzi uliofanyika mwaka huu na kusimamiwa na shirikisho hilo.
Ferdinand Chacha na Ali Kinduli ambao ni waamuzi wasaidizi ndiyo wapya katika jopo hilo la waamuzi wa FIFA kwa Tanzania. Waamuzi wa kati waliopata tena beji hizo ni Ramadhan Ibada, Orden Mbaga, Israel Mujuni na Sheha Waziri.
Mbali ya Chacha na Kinduli, waamuzi wengine wasaidizi kwa upande wa wanaume ni Josephat Bulali, Hamis Changwalu, Erasmo Clemence, Khamis Maswa na Samuel Mpenzu. Kwa upande wa wanawake, mwamuzi wa kati ni Judith Gamba wakati wasaidizi ni Mwanahija Makame na Saada Tibabimale.
Mwamuzi pekee wa FIFA 2011 ambaye jina lake halikurudi ni John Kanyenye ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.