Habari za Punde

*NHIF YAANZISHA KLABU YA MAZOEZI KWA WATUMISHI WAKE KILA J'MOSI KWENYE VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI OYSTERBAY

 Nahodha wa timu ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, akiongoza mazoezi ya wafanyakazi wa Mfuko huo ikiwa ni maandalizi ya kuzinduliwa kwa mpango maalum wa Klabu ya mazoezi kwa wafanyakazi ulioanza leo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Mazoezi hayo yatakuwa yakifanyika kila siku ya Jumamosi katika uwanja huo.
 Mazoezi yakiendelea kwa wafanyakazi wanawake kwa Wanaume.
Mazoezi ya kupasha misuli moto yakiendelea.
******************************************
MfFUKO wa Taifa wa Bima ya afya wajiandaa na uzinduzi wa klabu ya michezo kwa watumishi wake ili kuwapa fursa ya kulinda afya zao na magonjwa mabalimbali yanayotokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya kila siku kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengineyo mengi ambayo kwa sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu wa leo.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Oyesterbay, Meneja wa timu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu na Utawala Bi. Jane Nchimbi, alisema kuwa utaratibu huo ulianza tangu mwanzoni mwa mwaka jana ila ulishindwa kuwa endelevu kutokana na majukumu ya kazi.

 ''Tumekuwa na utaratibu huu tangu mwanzoni mwa mwaka jana lakini kidogo tulikuwa tumebanwa na majukumu, lakini kwa sasa tumeamua kwa pamoja kuanza utaratibu huu kuwa endelevu kwani utasaidia kujenga afya hasa ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa Umma  tunatumia muda mwingi maofisini tkuhudumia wateja hivyo kuwa na nafasi finyu kushiriki mazoezi kama ambavyo NHIF tumethubutu.

Pia mpango huu unawajumuhisha pia wale watumishi wa Mfuko kwenye ofisi  za Mkoani, mpango wa baadaye ni kuwa na eneo maalum la kufanyia mazoezi (gym) ili huduma zote za msingi ziweze kupatikana.'' alisema Bi Jane kijazi

Naye nahodha wa timu ya mpira wa pete  ya NHIF bi Sabina Komba, aliwataka wafanyakazi wanaoshiriki mazoezi kwenye klabu hiyo kutambua kuwa wao ni mabalozi katika kuhamasisha wananchi na wananchama wa mfuko huo kupenda na kuthamini michezo kwani mfumo wa maisha ya kisasa umegubikwa na maradhi mengi na  makubwa ambayo yanaathiri afya zetu na walio wengi
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.