Baadhi ya Mashabiki wa Yanga walifika Klabuni hapo mtaa wa Jangwani leo mchana kwa lengo la kumuondosha madarakani Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Lloyd Nchunga, wakihamaki na kuhamasisha kuanza kwa zoezi hilo. Mashabiki na wanachama hao wa Yanga wamefikkia hatua hiyo kutokana na kuona timu yao ikiboronga katika Ligi Kuu iliyomalizika wiki iliyopita huku timu hiyo ikimaliza vibaya kwa kukubali kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya watani wao wa Jadi Simba.
Mmoja kati ya mashabiki waliokuwapo eneo hilo, akiwa ametiwa nguvuni na askari kufuatia vurugu za kuchapana wenyewe kwa wenyewe Klabuni hapo.
Askari akilinda usalama mahala hapo.
Wanachama hao wakiwa nje ya Jengo la Klabu hiyo wakimsubiri Lloyd Nchunga.
Askari wakilinda usalama nje ya Jeno hilo.
No comments:
Post a Comment