Habari za Punde

*MSIBA, MHARIRI WA MTANZANIA MICHEZO, RACHEL MWILIGWA AFARIKI DUNIA

Rachel Mwiligwa enzi za uhai wake, akiwa katika majukumu ya kazi.

Aliyewahi kuwa mwandishi wa michezo wa Gazeti la Bingwa na Mtanzania na hadi kifo chake alikuwa ni Mhariri za Gazeti la Mtanzania upande wa Michezo, Rachel Mwiligwa, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mwananyamal, alikokuwa amelazwa kwa kipindi kirefu akisumbuliwa na maradhi.

Rachel, anatarajia kuzikwa siku ya Jumatatu baada ya taratibu za maziko kukamilika, na shughuli za msiba huo, zinafanyika maeneo ya Goba, eneo ambalo mpaka sasa halijajulikana. Kwa taarifa zaidi waweza wasiliana na Mpiga Picha Mkuu wa New Habari, Anthony Siame kwa Namba, 0713 403248 kwa maelekezo zaidi kuhusu shughuli zote za msiba kwani kama Ofisi ikingali ikifanya taratibu za kutoa taarifa za ratiba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.