Habari za Punde

*BREAKING NEWZZZ!!!! PROF. GEORGE SAITOTI AFARIKI DUNIA NCHINI KENYA


Waziri wa Usalama wa ndani wa Kenya, Profesa. George Saitoti, (pichani) amefariki dunia kwa ajali ya Helikopta, aliyokuwa akisafiria akiwa katika safari ya kikazi akielekea Kisumu, akiwa na Naibu Waziri wake Orwa Ojode na kupata ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Ngong, nchini humo na kufariki dunia.

Habari zilizoufikia mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, zinasema kuwa ajali hiyo, imetokea katika maeneo hayo ya Ngong, katika milima ya Magharibi mwa Jiji la Nairobi nchini nchini Kenya.

Mpaka sasa bado Serikali ya Kenya haizungumzia ajali hiyo iliyowapoteza Waziri na Naibu wake pamoja na watu wanne na kufanya jumla waliofariki katika ajali hiyo kufikia watu Sita.

Profesa Saitoti, alikuwa ni mmoja kati ya watu waliojitokeza kutangza kugombea urais katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika hivi karibuni nchini humo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.