Habari za Punde

*MASHABIKI WA CHELSEA WA TANZANIA, KUSHEREHEKEA KOMBE LA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Rodrick Mwambene akisisitiza jambo katika kikao hicho cha mashabiki wa timu ya Chelsea, kuhusu maandalizi ya sherehe ya kusherehekea kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
************************************
Na Mwandishi wetu
Kufuatia mafanikio makubwa ya timu ya Chelsea kwa kutwaa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mashabiki wa Tanzania wa timu hiyo wameandaa sherehe kubwa ya kusheherekea ubingwa huo iliyopangwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Mashabiki hao kupitia kamati yao maalum walifanya kikao jana kwenye hotel ya Wanyama, Sinza Mori na kukutwa na blogu yetu. Kamati hiyo imeundwa na wadau mbali mbali chini ya mwenyekiti, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la kandanda nchini, TFF, Fredrick Mwakalebela, Afisa Habari wa zamani wa TFF, Florian Kaijage na mpenzi mkubwa wa michezo wa timu hiyo, Rodrick Mwambene.
Wengine wanaunda kamati hiyo ni Mmiliki wa kituo cha redio cha Times, Lehure Nyaulawa, Mtangazaji wa Times FM, Clifford Ndimbo, Deogratius Rweyunga, Peter Ngassa na wengine mbali mbali.
Wadau hao walisema kuwa wana mipango mikubwa ya kuendeleza umoja wao na Jumatatu watafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mipango hiyo.
Walisema kuwa lazima wafanye sherehe ya ‘kufa mtu’  na wanataka kumwalika mmoja wa wachezaji wa timu hiyo kuhudhuria sherehe hiyo ya kwanza nay a aina yake hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.