Habari za Punde

*RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI OTTAW, CANADA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akitambulishwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akisaini katika kitabu cha wageni Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini humo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo. Jumba hilo ni makazi  na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada kuanzia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi katika jumba hilo, pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, na pia ni mahala pa  kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje pia ni mahala anapoanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na watanzania walijitokeza kumpokea akiongozana na Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson, katika viwanja vya jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na  Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson, kuingia  jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini humo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.