Habari za Punde

*BAADA YA KUSHINDWA KUTWAA HATA NAFASI YA 3 TIMU YA KILIMANJARO STARS KUREJEA LEO NCHINI


TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, iliyokuwa inkishiriki michuano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, Uganda inarejea Dar es Salaam leo Jumapili (Desemba 9, 2012).
 
Timu hiyo  inatarajia kutatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere   majira ya saa 11 kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir.
 
Baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kumaliza kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu (Desemba 10, 2012) saa 6 kamili mchana ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) atatangaza kikosi chake kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.