MAANDALIZI ya pambano la
Masumbwi kati ya Francis Cheka na bondia Chiotka Chimwemwe, kutoka Malawi, litakalochezwa Desemba 26
mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
yamekamilika.
Akizungumza na mtandao huu, jijini Dar es Salaam, promota wa pambano hilo
Andrew George ,amesema taratibu zote za maandalizi ya mchezo huo huo wa kimataifa zimekamilika.
"Taratibu zote
za pambano zimekamilika kwa asilimia 90 ikiwa ni pamoja na kumtumia tiketi bondia
Chiotka Chimwemwe", alisema George.
George alisema ameamua kulipeka
pambano hilo Arusha kwa kuwa anaamini kuwa ni kipindi kirefu sasa kwa wakazi wa jijini Arusha na wapenzi wa mchezo wa ngumi, hawajapata kushuhudia mchezo huo.
Na tumeonelea kupanga pambano hili siku ya Sikukuu ili watu wengi waweze kujitokeza kushuhudia ndonga za Cheka kwani ni muda mrefu hawajamuona akifanya vitu vyake na pambano linatarajia kuanza mishale ya saa nan mchana''. alisema George
Pia alisema mabondia watapima uzito siku ya sikukuu ya krismasi jijini Arusha.
Pambano hilio litakuwa ni la raundi 12 na Mmalawi huyo anajigamba atampiga Cheka ndani ya ardhi ya nchi yake hivyo nawaomba Watanzania kuja kwa wingi kumsapoti bondia wetu na ulinzi utakuwepo wa kutosha, alisema George.
No comments:
Post a Comment