Habari za Punde

*PUSH MOBILE YAKABIDHI ZAWADI ZA PIKIPIKI KWA WASHINDI WA SERENGETI FIESTA

 Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rodney Rugambo akikabidhi namba ya usajili ya pikipiki kwa mshindi wa bahati nasibu ya Serengeti Fiesta, Boniface Magambo  katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Kinondoni jana ambapo Jumla ya pikipiki 14 zenye thamani ya sh milioni 20 zilikabidhiwa kwa washindi baada ya kushindikana kukabidhi wakati wa tamasha hilo kutokana na malipo ya ushuru. Picha/ Mpigapicha wetu.
************************
Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kimya cha muda mrefu,  hatimaye kampuni ya Push Media Mobile Limited imekabidhi zawadi za pikipiki 14 zenye thamani ya sh. Milioni 20 kwa washindi wa mwaka huu wa tamasha la  Serengeti Fiesta.
Kampuni hiyo ilishindwa kukabidhi zawadi hizo awali kutokana na sababu kuu moja ambayo ni malipo ya ushuru (kodi) za  kuingiza pikipiki hizo hizo nchini na kufanya zoezi hilo kuchelewa.
 
Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rodney Rugambo alisema kuwa kampuni yao imekabidhi pikipiki mpya kwa washindi hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali ambayo taamsha la fiesta lilifanyika.
 
Washindi hao ni  Irene Stevens na WilliamMgala wote kutoka Dar es Salaam, Rashid Juma Ramadhani (Tanga), Nasiru Habibu, Michael Swai (Mara),  Veronica Mandisi, Mchungaji Amos Kurubone wa Shinyanga.
 
Rugambo aliwataja washindi wengine kuwa ni Mwanahamisi Msangi (Tabora), Thadey Kiwale (Singida), Joseph Nashon Magambo,  Reinatus Waitura (Morogoro) na Ali Muhamed Sanga na Christopher Mtibwa wa Iringa.
 
Alisema kuwa kukabidhi zawadi kwa washindi hao kunafanya kukamilika kwa zoezi hilo kwa mwaka huu ambapo zawadi kubwa ya magari mawili yalikwenda kwa  Diana Elisa Mkoba  yenye thamani ya shs milioni 16.
 
Kampuni hiyo ilitoa gari moja moja mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza na Dodoma. Mbali ya zawadi hizo, kampuni hiyo pia ilitoa zawadi za simu ya mkononi aina ya Nokia dabodabo 130, simu aina ya blackberry 14 na washindi wa fedha taslim shs milioni 20. Thamani ya zawadi zote ni milioni 200.
 
“Ni matarajio yetu kuwa washidni watatumia pikipiki ipasavyo na kujiongezea vipato, watu wengi walishiriki katika bahati nasibu hii na wenye bahati ndiyo walioshinda, tunawaomba wadau washiriki katika promosheni zetu nyingine,” alisema Rodney.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.