Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema katika Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Mazingira wa Afrika (AMCEN) uliofanyika mjini Kampala Julai 2002, ulibaini kuwa ukosefu wa taarifa za hali ya mazingira katika bara la Afrika ni moja ya sababu zinazochangia mipango duni ya usimamizi wa shughuli za maendeleo na utekelezaji Mikataba ya Kimataifa ya utunzaji mazingira.
Amesema kutokana na hali hiyo AMCEN iliiomba UNEP wafadhili program ya Afrika ya Mtandao wa Hali ya Mazingira (Africa Environmental Information Network) ili kuongeza uwezo wa nchi za Afrika wa kuwa na Taarifa za Hali ya Mazingira na Mtandao wa Habari baina ya nchi za Afrika.
Mh. Huvisa ameweka wazi kuwa taarifa hiyo imekamilika na iko tayari kwa ajili ya utekelezaji, na kuwa taarifa hiyo imeezea Historia ya jiji la Dar es Salaam, Jiografia na Fiziolojia yake, suala la uchumi Jamii, Sera, Sheria na Mfumo wa Utawala Kimazingira, Usimamizi wa Rasilimali ya Ardhi, Rasilimali Maji, Madini na Nishati, Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira, Uchafuzi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi. (Picha zote na Mo Blog).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam akisema Tanzania ni moja ya nchi zinazotekeleza program ya mtandao wa taarifa za hali ya mazingira yaani “Africa Environmental Information Network (AEIN) chini ya ufadhili wa Shirika la Mpango wa Mazingira Duniani (UNEP).
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot akizungumza kabla Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa hajazindua Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema taarifa hiyo ina mapendekezo makuu 12 na kutoa wito kwa serikali ya Tanzania kutafakari kila pendekezo sambamba na kuzitumia taarifa za kimazingira kwa manufaa ya taifa.
Afisa Mwakilishi wa UNEP Tanzania Clara Makenya akizungumza machache kabla ya kuzinduliwa kwa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam na kusisitiza kuwa UNEP inatambua umuhimu wa kuwa na ripoti kama hiyo, hivyo amewataka wahusika kuipitia na kuielewa kwa makini na utekelezaji wa yalimo uanze kwa muda muafaka.
Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Abdallah Chaurembo akitoa neno la shukrani kwa wafadhili wa Programu ya Mazingira wakati hafla ya uzinduzi wa taarifa ya hali ya Mazingira ya jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa akikata utepe kuzindua rasmi taarifa ya hali ya Mazingira ya Jiji la Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kushoto) Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot (wa tatu kulia), Afisa Mwakilishi wa UNEP Tanzania Clara Makenya (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava ( wa kwanza kulia).
Sasa imezinduliwa rasmi.
Pichani Juu na Chini ni Maafisa Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wakurugenzi, wawakilishi wa vyombo vya habari , Wakurugenzi wa Manispaa za jiji na Wadau wa Mazingira waliohudhuria halfa ya uzinduzi wa taarifa hiyo.
Mgeni rasmi Dkt. Therezya Huvisa akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa UNEP/UNDP pamoja na wadau wa Mazingira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Phillipe Poinsot pamoja na Afisa Mwakilishi wa UNEP Tanzania Clara Makenya baada ya uzinduzi taarifa ya hali ya mazingira ya jiji la Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Taifa cha Utalii jijini Dar leo.
No comments:
Post a Comment