KAMPUNI ya Lakeland Africa kesho
itaanza safari ya ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ kwa siku 14 kwa lengo la kukuza
utalii wa ndani na kujenga utamaduni wa Watanzania kutembelea vivutio vya utalii
nchini.
Safari hiyo itakayoanzia Mlimani City Dar es Salaam
kesho inatoa fursa kwa watanzania kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo Hifadhi
ya Saadan, Pangani, Lushoto, Tarangile, Olduvai Gorge, Lake Manyara, Ngorongoro
na Serengeti na pia watapata nafasi ya kutembelea kijiji cha Butiama
alikozaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere na kuzuru katika kaburi
lake.
“Lakeland Africa sasa itaendesha safari za namna hii
kuhimiza watu kutembelea vivutio vya utalii nchini kwa kauli mbiu ya ‘kuwa
mtalii ndani ya nchi yako”
Kuanzia mwezi januari mwakani Lakeland Africa itaendesha
safari za kila wiki kwenda hifadhi na makumbusho ya kistoria katika maeneo
mbalimbali hapa nchini ikiwamo Lushoto, Pangani, Saadani, Selous, Kilwa,
Bagamoyo na Mikumi
Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata fursa hii
ya kuitembelea nchi yake Lakeland Africa imeandaa ratiba ya mwaka mzima ya
safari zote ili watu waweze kuchagua na kupanga safari kulingana mahitaji
yao.
Wapigie Lakeland Africa sasa kupanga safari yako ya
mwakani, mwezi wowote utaopenda kuzuru na kuwa mtalii ndani ya nchi
yako.
metolewa na Lakeland
Africa.
+255222-761811
+255784885901
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi
yako’
No comments:
Post a Comment