Mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kusalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot.
Pichani Juu na Chini ni maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu yaliyohusisha Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali, Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu yakiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Meza Kuu ikipokea maandamano ya Wanafunzi na Taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali wakati sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu zilizofanyika jijini Dar leo.
Jaji Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento akisoma hotuba yake katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu ambapo aliwasilisha Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa nchi zote zihakikishe kuwa zinafuata maazimio ya tamko la haki za binadamu na wananchi wake wanufaike na haki zilizomo ndani yake.
Mwanasheria Mkuu wa Sreikali Jaji Frederick Werema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambapo amesema chini ya mpango wa pamoja, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unasaidia vitengo muhimu vya serikali na wadau wengine wa mzunguko wa Haki za Binadamu, kwa mfano ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na idadi kubwa ya Asasi zisizo za kiserikali zinazohusika na masuala ya Haki za Binadamu.
Vilevile amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuinga mkono serikali kufuatilia ahadi zilizotolewa kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na mapendekezo yakiwemo kutoka katika Bodi za Mikataba ya haki za Binadamu.
Afisa Mipango kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Abdu Mohammed akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ambapo amesisitiza kila raia anapaswa kuwa na haki na fursa ya kushiriki katika masuala ya umma, moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi huru wa kuchaguliwa, pia kila binadamu ana haki ya kupiga kura na kuchaguli na na kuweza kufikia huduma za kijamii sambamba uhuru wa kujieleza, kukusanyika na kuungana.
Amongeza kuwa haki hizi zinatakiwa kumhusu kila mtu na hakuna hata mmoja atakaye baguliwa kwa moja kati ya hizo kwa sababu ni mwanamke, au anatoka katika kundi dogo, au anaabudu katika dini Fulani, au kwa sababu ni shoga, au ana ulemavu, anaamini siasa Fulani, au mkimbizi au ana rangi fulani, anatoka katika kabila Fulani.
Mgeni rasmi Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisoma hotuba yake ambapo amesema Pamoja na kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Haki za Binadamu, pia tunaadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa pamoja. Kaulimbiu ya mwaka huu katika Kupambana na Rushwa ni “Unaweza kuzuia rushwa, chukua hatua sasa”. Kauli hii inaonesha umuhimu wa Wananchi wa rika zote kupiga vita rushwa.
Mh. Pinda amesema hatua ya kuunganisha maadhimisho haya na kufanyika sehemu moja kunapunguza gharama kwa upande wa Serikali, na pia kunatoa nafasi kwa Wananchi kufahamu umuhimu wa siku zote mbili bila kulazimika kuondoka eneo moja la tukio kwenda eneo jingine. Napenda kuzipongeza Taasisi zote husika kwa kuunganisha matukio haya mawili na kuadhimisha sehemu moja na kwa wakati mmoja.
Ameongeza kuwa Huu ni mwaka wa tano tangu Taifa letu lilipoanza kuadhimisha siku hii Kitaifa. Kaulimbiu ya Kimataifa kwa mwaka huu ni: “Sauti yangu inachangia” (My voice counts). Ujumbe huu unatukumbusha kushiriki katika kutoa maoni katika shughuli mbalimbali za Kijamii au Kitaifa.
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto) na Naibu wake Mh. Angellah Kairuki (kulia).
Sasa imezinduliwa rasmi....Mh. Waziri mkuu Pinda akionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani). Kulia ni Jaji Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento na Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto).
Waziri Mkuu Pinda akipitia ripoti hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akipitia nakala taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kikundi cha Wana wandime ya kwetu ngoma wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Pichani Juu na Chini ni Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za serikali, Wanafunzi wa shule za Sekondari, Wadau wa Haki za Binadamu na Wananchi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Waziri wa Katiba na Sheria na Naibu wake.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu huku akisindikizwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment