Habari za Punde

*POULSEN AITA 24 STARS, CANAVARO AREJESHWA KUMPA TAFU YONDANI

 
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars, jana alitaja kikosi kamili kitakachoingia kambili leo, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo  wa kirafiki dhidi yao na mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolipolo) mchezo unatarajia kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Desemba 22, mwaka huu.
 
Miongoni mwa wachezaji walioitwa katika Kikosi hicho ni pamoja na Beki wa Yanga ya Dar es Salaam na timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Nadir Haroub 'Canavaro' kwa ajili ya kusaidia na katika safu ya ulinzi na Kelvin Yondani.
 
Akizungumza na waandisi wa habari, katika ofisi za TFF jijini Dar jana, Kocha Kim, alisea kuwa ameamua kuingiza sura mpya katika kikosi hicho, baada ya kuona uwezo wa wachezaji hao ulioonyeshwa wakati wa michuano ya Challenge, yaliyomalizika hivi majuzi huko, nchini Uganda na yale ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Visiwani.
 
Kim, alitaja Kikosi kamili kilichoitwa kuwa ni pamoja na makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Simba).
Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC).
 Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

 Wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji wa Azam, Mcha Khamis.

Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kamapala, Uganda. Wachezaji hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.

WAKATI HUO HUO ZAMBIA YATAJA KIKOSI CHA KUIVAA STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Zambia (Chipolopolo) ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.

Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.