Habari za Punde

*MHE. RAISI JAKAYA KIKWETE AFURAHIA UJIO WA WINGS OF KILIMANJARO

Rais JK akiwa na meneja wa Wings of Kilimanjaro jijini Arusha.
Wings of Kilimanjaro, tukio linalotokea mara moja katika maisha inategemea kufanyika mwishoni mwa Januari 2013, itategemea kupata kiasi cha watu 200, watalaamu wa spoti inayoitwa ‘paragliding’ and ‘philanthropists’ wakitembea mpaka kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Nia ya tukio hili ni kupata jumla ya dola million moja ambayo itasaidia taasisi tatu zinazofanya kazi ya kusaidia jamii hapa nchini Tanzania, ambazo ni ‘Plant With Purpose’, ‘One Foundation’ na ‘World Serve International’.
 
  Katika siku ya uzinduzi, wataalamu wa paragliding (ikiwemo wale amabyo wanajulikana duniani) na abiria wao watazindua siku hiyo na kwenda mkoani Kilimanjaro. Muda wa kuruka angani mpaka Moshi itatumia dakika 40.  
Mapema wiki iliyopita, Meneja wa Wings of Kilimanjaro, Bi Paula McRae alipata nafasi yakukutana na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, katika safari yake huko mkoani Arusha.

Akiwa katikia mazungumzo na Rais, Bi. Paula, alizungumzia kuhusu tukio la Wings of Kilimanjaro, ambapo Mhe.Rais, alifurahi sana na kuwashukuru  timu ya Wings of Kilimanjaro kwa kutoa ushirikiano kwa njia ya juhudi ya kutafuta fedha na pia kuweza kupromote Mlima Kilimanjaro ulimwenguni. 
Aidha Rais, aliendelea kutambua habari katika vyombo vya habari ikizugumzia boti ya Mt. Kilimanjaro, ambayo ilikuepo London, nchini Uingereza (zaidi ya watu milioni 20 wanaangalia katika kipindi cha BBC), pia iliweza kutoka kwenye magazine ya National Geographic na pia kupokelewa na balozi wa hiari, Doug Pitt.

  Timu ya Wings of Kilimanjaro wanafurahia kuwaonyesha Watanzania, mchezo ambao haijulikani sana nchini, inayoitwa ‘paragliding.

Timu ya Wings of Kilimanjaro itatoa ushindani tukikaribia katika tukio, wa Tanzania wawili wataweza kusafiri na rubani wa paragliding mwezi wa pili.

1 comment:

  1. This is super exciting! Floresta Tanzania, Plant With Purpose's Tanzanian NGO partner, will be pleased to host these pilots and to plant a million trees as a result of this amazing event!

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.