Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyepata kutamba siku za nyuma na vibao vyake kadhaa hapa nchini, Rehema Chalamila, 'RAY C', jana alitinga Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa msaada wa matibabu aliopatiwa wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Ray C, alifika Ikulu akiwa amefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve, ambapo alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake kama kawaida.
Naye Mama Mzazi wa Ray C alimshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.
No comments:
Post a Comment