Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo 'Wazee wa Kizigo', Ally Choki
na Kiongozi wa Shoo wa bendi hiyo, Super Nyamwela, wameondoka nchini wiki
iliyopita kuelekea nchini Japan kwa ajili ya kufanya maonesho kadhaa binafsi
nje ya bendi hiyo.
Akizungumza na Mtandao huu, kabla ya
kuondoka nchini Ally Choki, alisema kuwa wamepata mwaliko kama watu binafsi na
si kundi zima, jambo ambalo limewalazimu kusitisha maonyesho yao ya kawaida
hapa nchini kwa muda ili kukamilisha safari hiyo inayotarajia kuwa ni zaidi ya
miezi mitatu.
![]() |
| Nyamwela akipozi huko umangani. |
Wakiwa nchini Japan, wanatarajia kufanya
maonyesho kadhaa waliyoandaliwa na mwenyeji wao, wakiwa na bendi iliyoandaliwa
kufanya nao mazoezi maalum kwa ajili ya shoo hizo, ambapo pia wanatarajia
kufanya shoo na mwanamuziki mahiri wa siku nyingi anayepiga kazi zake nchini
humo, Fresh Jumbe.
Aidha Choki alisema kuwa kwa kipindi chote
watakachokuwa nje ya Nchi Wanamuziki wa bendi yake watakuwa likizo kutokana na
mashabiki walio wengi wa muziki wa dansi kutoamini bendi bila kiongozi au Staa
wanayempenda kuwepo.
''Naogopa kuwaachia bendi wanamuziki wangu
yasije yakawakuta yale yaliowahi kuwakuta wanamuziki wa Christian Bella, huko
Kimara ambapo walizua mtafaruku mkubwa baada ya kutaka kupiga shoo bila kuwepo
Bella huku mmoja akivaa Pama na kujifanya ni Bella na aliposhitukiwa alivuliwa
pama na kushambuliwa na mashabiki jambo lililozua mtafaruku mkubwa na
kusababisha kuvunjika kwa baadhi ya vyombo, ndiyo maana mimi nimeamua kusitisha
maonyesho'', alisema Choki
Kiongozi wa Shoo wa bendi hiyo, Super Nyamwela (kulia) akiwaongoza wenzake kushambulia jukwaa katika onyesho la mwisho la bendi hiyo kabla ya kutimkia nchini Japan, hivi majuzi.
*********************************
Kabla ya kuondoka nchini Choki, aliitisha
kikao cha dharula na kuwatangazia wanamuziki wake kuwa bendi hiyo imeamua
kusitisha maonesho yake kwa muda, ambao haukutangazwa mwisho wake na kuwataka
wasanii wote wanaounda bendi hiyo kufanya ustaarabu mwingine kwa kipindi hicho
chote.
Baadhi ya wadau wa muziki nchini wamesema
kuwa bendi hiyo haikuwa ikifanya vizuri na katika maonyesho yake ya hivi
karibuni, huku Mkurugenzi wake Ally Choki, akionekana kutokuwa na mudi ya
kufanya kazi na hasa tangu alipoondokewa na mke wake kipenzi mwaka jana.
Wanenguaji wa kike wa bendi hiyo, wakiwajibika jukwaani katika onyesho lao la mwisho kabla ya kuitishwa kikao cha kutangaziwa kufungwa kwa muda bendi hiyo.
******************************
''Inawezekana kifo cha mkewe ndiyo sababu
kubwa ya kuyumba kwa bendi hiyo, na hasa kwa Choki ambaye muda mwingi
alionekana kutokuwa na raha muda mwingi tangu alipofiwa na mkewe na hivyo
kushindwa kufanya kazi kama alivyokuwa zamani ili kuwaridhisha mashabiki
wake'', alisema mdau huyo wa muziki, aliyejitambulisha kwa jina la Kantoka
kutoka Home Allone Kinondoni
Baadhi ya waimbaji wa bendi hiyo siku walipofanya onyesho lao la mwisho kabla ya Viongozi wao kuwatangazia kusimamisha maonesho ya bendi hiyo kwa muda usiojulikana.





No comments:
Post a Comment